Habari kutoka nchini Mali zinaeleza kuwa shambulio iliyowaua watu kadhaa
imefanyika eneo la Mgahawa ambapo raia wa mataifa ya Magharibi
walikuwako.
Wapiganaji wa Kiislaam walikivamia
kwa nguvu katikati mwa mji wa Bomako iliyo mji mkuu wa nchi ya
Mali,walioshuhudia wamesema Mghahawa waliokuwepo Raia hao wa kigeni
ambapo baadhi yao ni kutoka Ubilgiji na France walishambuliwa na watu 5
wameuawa.
Afisa mmoja
aliyezungumza kwa niaba ya U.N amesema wanaume hao waliotekeleza
shambulio hilo walitumia Mabomu ya kurusha kwa mkono na kisha kuanza
kuwaua watu mmoja baada ya mwingine ndani ya Mghahawa hiyo.
Msemaji wa Polisi mjini Bomako
amethibitisha kuwa watu waliotekeleza shambulio hilo wamefanikiwa
kuondoka kwa Gari dogo na hakuna aliyewafuatilia.
Mali ilivamiwa
na Wanajeshi kutoka Ufaransa wakisaidiwa maelfu ya Wanajeshi kutoka
Afrika mwaka 2012 huko hali ya usalama katika nchi hiyo ikiwa tete
wakati wapiganaji wa Kiislaam wakiwa na nguvu upande wa Kaskazini mwa
nchi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni