Namuomba
Allaah Mtukufu, Mola wa 'Arshi kubwa Akutawalishe katika dunia na
Akhera na Akufanye wewe uwe mwenye baraka popote utakapokuwa na Akufanye
wewe uwe miongoni mwa wale wanapopewa wanashukuru, na wanapopewa
mitihani wanasubiri, na wanapofanya madhambi huomba msamaha, hakika haya
mambo matatu ni anwani ya kufaulu.
Jua,
Akuongoze Allaah katika kumtii Yeye, hakika kumpwekuesha Allaah ni mila
ya Nabii Ibraahiym ('Alayhis Salaam) nayo ni kumuabudu Allaah peke Yake
hali yakuwa ni mwenye kumtakasia dini kama alivyosema Allah:
"Na wala Sikuwaumba Majini na Wanaadamu ila kwa lengo la kuniabudu Mimi" Adh-Dhaariyaat: 56.
Basi
pindi takapofahamu kuwa hakika Allaah Amekuumba wewe kwa lengo la
'Ibaadah, itakupasa ujue ya kwamba 'Ibaadah haiitwi 'Ibaadah mpaka
ipatikaniwe kumpwekesha Allaah, kama ilivyo Swalah haitwi Swalah mpaka
ipatikaniwe twahara basi itakapoingia shirki katika 'Ibaadah inaharibika
'Ibaadah kama hadathi inapoingia katika twahara inaharibu twahara, basi
utakapojua hakika ya shirki itakapochanganyika na 'Ibaadah inaiharibu
'Ibaadah na inaporomosha 'amali na atakuwa huyo aliyemshirikisha Allaah
katika moto milele basi utakuwa umejua ya muhimu kwako ni kulijua hilo
ili huenda Allaah Akuokoe na mtego huu nao ni kumshirikisha Allaah,
shirki amabayo Allah Alisema kuhusiana nayo:
"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa pamoja naye na anasamehe kwa yalio kuwa chini ya shirki kwa amtakaye" An-Nisaa: 116
Nayo ni kwa kujua misingi minne alioitaja Allaah katika kitabu Chake.
MSINGI WA KWANZA
Ni
kujua ya kwamba wale makafiri aliopigana nao vita Mtume Muhammad
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wanakubali ya kwamba Allaah
Mtukufu ndio muumbaji mwenye kupeleka mambo lakini kuamini huko
hakukuwaingiza katika Uislamu na ushahidi ni neno lake Allaah:
"Sema
(ewe Muhammad, uwaambie hao washirikina) ni nani anayewaruzu kutoka
mbinguni na ardhini, na ni nani anayemilki kusikia kwenu na kuona kwenu,
na ni nani anayetoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na ni nani
apelekaye mambo? Basi watasema ni Allaah sema (kuwaambia) basi
hamumuogopi Allaah?" Yuunus: 31
MSINGI WA PILI
Ni
ya kwamba wao washirikina wanasema hatuwaombi na wala hatuwaelekei kwo
hao waungu wao ila kutaka kukurubishwa na kutaka uombezi kwa Allaah na
ushahidi ya kwamba wao walikuwa wakiwaabudu kutaka kukurubishwa ni neno
Lake Allaah:
"Na
wale ambao waliofanya pasi na Allaah vipenzi wakidai hatuwaabudu ila
twataka watukurubishe kwa Allaah hakika Allaah Atahukumu katika yale
waliyokuwa wakitofautiana, hakika ya Allaah Hamuongozi yule ambaye ni
mkanushaji aliyekufuru" Az-Zumar: 3
Na dalili ya kutaka uombezi neno Lake Allaah Mtukufu:
"Na
wanaabudu asiyekuwa Allaah yule ambaye hawawadhuru wao wala
hawawanufaishi wao na wanasema hawa ndio vipenzi vyetu mbele ya Allaah" Yuunus: 18
Uombezi Uko Aina Mbili:
1) Uombezi uliokatazwa
2) Uombezi uliothibitishwa au kukubaliwa.
Ama uombezi uliokatazwa ni ule ambao unaoombwa kwa asiyekuwa Allaah katika yale ambayo hana uwezo juu yake isipokuwa Allaah tu na ushahidi ni neno Lake Allaah Mtukufu:
"Enyi mlioamini toeni Alikivyokuruzukuni Allaah kabla haijakufikieni Siku ambayo hapatakuwa kujikomboa ndani yake wala urafiki wala uombezi na waliokufuru ndio madhalimu" Al-Baqarah: 254
Na
uombezi unaokubalika ni ule ambao huombwa Allaah na muombaji
amekirimiwa kwa kupewa uombezi na yule mwenye kuombewa ni yule
aliyeridhiwa na Allaah kauli yake na vitendo vyake baada ya kupata
idhini kama Alivyosema Allaah:
"Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini Yake Allaah" Al-Baqarah: 255
MSINGI WA TATU
Ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitokeza kwa watu wenye 'Ibaadah aina tofauti tofauti wengine wakiabudu Malaika na wengine walikuwa wakiabudu Manabii na
watu wema na wengine wakiabudu miti na mawe wengine wakiabudu jua na
mwezi na Mtume akapigana nao vita na wala hakuwatofautisha kwa vile
wanavyoviabudu, ushahidi wa haya ni neno Lake Allaah Mtukufu:
"Na pigana nao vita (Makafiri) mpaka kusipatikaniwe fitna (shirki) na dini yote iwe ni ya Allaah peke Yake" Al-Anfaal: 39.
Na dalili ya jua na mwezi ni neno Lake Allaah:
"Na
katika alama Zake ni usiku na mchana na jua na mwezi, basi msilisujudie
jua wala mwezi bali msujudieni Allaah Aliyeviumba hivyo ikiwa nyinyi
kweli mnamuabudu Yeye Allaah" Fusswilat: 37
Na dalili ya Malaika ni neno Lake Allaah Mtukufu:
"Na wala hatukuwaamrisheni nyinyi kuwafanya Malaika na Manabii kuwa waungu" Aal-'Imraan: 80
Na dalili ya Manabii ni neno Lake Allaah:
"Kumbukeni
Allaah Atakaposema 'Iysa mtoto wa Maryam je, wewe uliwaambia watu
nifanyeni mimi na mamangu waungu badala ya Allaah? Aseme ('Iysa) Wewe
umetakasika kuwa na mshirika haiwi kwangu mimi kusema lisilokuwa la
haki, ikiwa mimi ningalisema bila shaka ungelijua, unayajua yaliyomo
katika nafsi yangu na wala sijui yaliyo katika nafsi Yako, hakika Yako
ni mjuzi wa ghayb" Al-Maaidah: 116.
Na dalili ya watu wema ni neno Lake Allaah:
"Hao
ndio wale wanaowaomba wakitaka kwake kukaribiana na Mola wao walio
karibu sana na Mola wao miongoni mwao (na Allaah kama Malaika, wao
wanafanya haya haya), wanatumai rehma Zake na wanaogopa adhabu Zake
Allaah" Al-Israa: 57
Na dalili ya miti na mawe ni neno Lake Allaah:
"Je, mumewaona Laata na 'Uzah na yule Manaata wa tatu wa mwisho?" An-Najm: 19-20
Na
Hadiyth ya Abu Waaqid Al-Laythiy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema
tumetoka na mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda
katika vita vya Hanayn na sisi tukiwa tumesilimu karibuni na walikuwa
washirikina wana mkunazi wakitundika hapo panga zao kwa ajili ya kupata
baraka, mti huo ukiitwa Dhaatu Anwaat, tukapita katika mkunazi tukasema
ewe Mtume tufanyie na sisi huo mti wa Dhaatu Anwaat tupate baraka kama vile walivyonao hao Dhaatu Anwaat, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Mungu Mkubwa hakika mmesema maneno makubwa kama vile Banu Israaiyl walivyomwambia Muusa" At-Tirmidhiy.
MSINGI WA NNE
Hakika
washirikina wa sasa wamezidisha kufanya shirki kuliko washirikina wa
mwanzo kwa sababu washirikina wa mwanzo walikuwa wakifanya shirki wakati
wa raha na wakimtakasia Allaah 'Ibaadah wakati wa matatizo. Na
washirikina wa sasa shirki zao ni wakati wote sawa wawe katika raha au katika shida, na dalili ni neno Lake Allaah:
"Na wanapopanda katika meli (wakiwa katika misukosuko) humuomba Allaah na hali ya kuwa wakimtakasia yeye dini, lakini pindi wakiokolewa wakifika katika nchi kavu wanarudia kaika shirki zao" Al-'Ankabuut 65
Imetimia hapa hii Misingi Minne na Swala na Salamu ziende kwa Mtume Muhammad
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni