Muislamu
anapothibitika katika iymaan na taqwa, hubashiriwa Jannah wakati
anapofikwa na mauti: Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:
إِنَّ
الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ
عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا
بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٣٠﴾ نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ ﴿٣١﴾ نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ ﴿٣٢﴾
Hakika wale waliosema: “Rabb (Mola)
wetu ni Allaah.” Kisha wakanyooka; Malaika huwateremkia (wakati wa
kutolewa roho kuwaambia) kwamba: “Msikhofu, na wala msihuzunike, na
pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa (kwayo). “Sisi
ni marafiki walinzi wenu katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata
humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mnatayoyaomba. “Ni mapokezi kutoka kwa Ghafuwrir-Rahiym (Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu).” [Fusw-Swilat: 30-32]
humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mnatayoyaomba. “Ni mapokezi kutoka kwa Ghafuwrir-Rahiym (Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu).” [Fusw-Swilat: 30-32]
Kadhaalika,
Muislamu anahitaji kuthibitika katika neno la Tawhiyd ili asalimike
kaburini na aweze kujibu maswali matatu atakayoulizwa na Malaika wawili;
Munkar na Nakiyr.
عَنْ
الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى
اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر
شَهِدَ أَنْ لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه
فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ
الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ))) البخاري
وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة
Imetoka
kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa
Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu
akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha Illa-Allaah wa Anna Muhammadar-Rasuulu-Allaah" [Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah] hiyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah: “Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah”)). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Neno hilo limepigiwa mfano na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni kama mti mzuri:
عَنْ
ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) قَال: كُنَّا عِنْد رَسُول اللَّه صَلَّى
اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ((أَخْبِرُونِي عَنْ شَجَرَة تُشْبِه -
أَوْ - كَالرَّجُلِ الْمُسْلِم لاَ يَتَحَاتّ وَرَقهَا صَيْفًا وَلاَ
شِتَاء وَتُؤْتِي أُكُلَهَا كُلّ حِين بِإِذْنِ رَبّهَا)) قَالَ اِبْن
عُمَر: فَوَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة وَرَأَيْت أَبَا بَكْر
وَعُمَر لاَ يَتَكَلَّمَانِ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّمَ فَلَمَّا لَمْ
يَقُولُوا شَيْئًا. قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وآله
وَسَلَّمَ: ((هِيَ النَّخْلَة)). فَلَمَّا قُمْنَا قُلْت لِعُمَرَ: يَا
أَبَتَاهُ وَاَللَّه لَقَدْ كَانَ وَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة.
قَالَ: مَا مَنَعَك أَنْ تَتَكَلَّم؟ قُلْت: لَمْ أَرَكُمْ تَتَكَلَّمُونَ
فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّم أَوْ أَقُول شَيْئًا. قَالَ عُمَر: لَأَنْ
تَكُون قُلْتهَا أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ كَذَا وَكَذَا - البخاري
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye
amesema: "Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) akauliza: ((Niambieni kuhusu mti unaofanana na au kama Muislamu,
ambao majani yake hayaanguki wakati wa majira ya joto, wala wakati wa
majira ya baridi, na hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Mola
wake)). Ibn ‘Umar akasema: “Niliufikiria kuwa ni mtende, lakini niliona
vibaya kujibu nilipoona Abu Bakr na ‘Umar hawakujibu”. Akasema Rasuli wa
Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Ni mtende)). Tulipoondoka,
nilimwambia ‘Umar: “Ee baba yangu! Wa-Allaahi nilihisi kuwa ni mtende”.
Akasema: “Kwa nini basi hukutaja?” Nikasema: “Nilikuoneni kimya,
nikaona vibaya kusema kitu”. Akasema ‘Umar: "Ungelisema, ingelikuwa bora
kwangu kuliko kadhaa na kadhaa” (Yaani ningelikuwa na fakhari zaidi
kuwa wewe mwanangu ndiye uliyeweza kujibu pekee). [Al-Bukhaariy]
Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) imethibitisha hayo Anaposema:
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ ﴿٢٤﴾ تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾ وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾ يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ ﴿٢٧﴾
Je,
huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno twayyibah (zuri) kama mti mzuri
mizizi yake imethibitika imara na matawi yake (yanafikia) mbinguni?
Unatoa mazao yake kila wakati kwa idhini ya Rabb (Mola) wake. Na Allaah
Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka (na kuzingatia). Na mfano
wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna imara.
Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa
dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah
Anafanya Atakavyo. [Ibraahiym: 24-27]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni