Watu waliokuwa wamejihami na silaha wamemwua Mbunge mmoja katika
Bunge la Serikali ya FG kwenye Wilaya ya Hamar Weyne mjini Mugadishu.
Walioshuhudia
wanasema katika Wilaya ya Hamar Weyne ameuawa Mbunge mmoja aliyetajwa
kwa jina la Mayow na mwanaume mwingine aliyewahi kuwa mbunge wakati wa
Utawala wa Sheikh Sharif.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa watu waliotekeleza mauaji hayo walikuwa na Gari na
baada ya kufikia malengo yao waliondoka katika eneo la tukio,Mashuhuda
wameleza kuwa Maaskari wawili pia waliauwa kwenye shambulio la Hamar
Weyne ambapo mmoja alikuwa ni Afisa mwenye cheo wa Ikulu ya Villa
Somalia.
Punde
tu baada ya shambulio hilo Harakat Al-Shabab Al Mujahideen ilizungumza
na vyombo vya habari na kuthibitisha kuhusika mauaji hayo,Sheikh
Abdulaziz Abuu Mus'ab Msemaji wa Kijeshi wa Al-Shabab ameliambia vyombo
vya habari kuwa vikosi vyao vilihusika kuwaua maofisa 3 na kumjeruhi
vibaya Mbunge mwingine wa Bunge la FG.
Ni
siku ya pili ambapo kuna mfululizo wa mashambulio ndani ya mji wa
Mugadishu,siku ya jana aliauwa Afisa mwenye cheo cha juu katika kitengo
cha Makachero wa Serikali ya FG.
Liban Jehow Abdi
SomaliMemo,Mugadishu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni