Habari kutoka Mkoa wa Jubba zinaeleza kuwa Ndege mmoja aina ya kivita
inayomilikiwa na Wanajeshi wa KDF waliofanya uvamizi katika Ardhi ya
Somalia imeharibika vibaya.
Mwandishi
wa habari aliyopo Mikoa ya Jubba ameliambia SomaliMemo kuwa Ndege ya
kivita aina ya MIG imeanguka eneo iliyo na umbali wa KLM 50 kutoka mji
wa Kismaayo na Marubani wawili wa ndege hiyo wameuawa.
Afisa
mmoja wa Harakat Al-Shabab Al Mujahideen amethibitisha kuwa kikosi chao
cha anga wamefanikiwa kudungua ndege ya kivita wakati ambapo ilikuwa
ikifanya mashambulio kutoka angani katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa
Lower Jubba.
Wakaazi
wamesema waliona moto ukiwaka eneo iliyoangukia Ndege hiyo ambayo ni
eneo linalojulikana Daseg-Wamo ulio umbali wa KLM 50 kwenda mji wa
Kismaayo.
Fuatilia yatakayojiri
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni