| mjini baydoa |
Kuna maelezo zaidi kuhusiana na mlipuko mkubwa uliosababisha hasara
ambao ulifanyika jana katika mji wa Baydoba makao makuu ya mkoa wa Bay.
Takriban
watu 12 wamepoteza maisha kufuatia milipuko miwili huko watu wengine 35
wakijeruhiwa vibaya katikati mwa mji wa Baydoba,wengi wa waliouawa
kwenye mlipuko huo ni wanasiasa pamoja na wazee wanaowakilisha mikoa
mitatu yaliojitangazia kujitawala.
Duru
zinaeleza kuwa majeruhi wa shambulio hilo waliolazwa jana usiku katika
Hospitali kuu ya mji wa Baydoba wamepoteza maisha usiku wa manane.
Hassan
Lug Guur ambae alkuwa mwenyekiti wa mkutano wa Mikoa mitatu alijeruhiwa
vibaya kwenye shambulio hilo huko makamu wake akiuawa kutokana na mkasa
huo.
Vyanzo
muhimu vilieleza kuwa mmoja wa mashambulio hayo ililengwa mkutano
uliokuwa ukiendelea kwa maofisa wa Utawala wa Jimbo la Bay na Bakool
ambae mkuu wake akiwa Sharif Hassan anae fanya kazi na Ethiopia.
Liban Jehow Abdi
SomaliMemo,Mugadishu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni